NAIBU WAZIRI SHONZA MGENI RASMI TANAPA LUGALO OPEN 2019 | ZamotoHabari

Na Luteni Selemani Semunyu

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh Juliana Shonza anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufungaji mashindano ya TANAPA Lugalo Open  Mashindano yanayotarajia kutimua Vumbi kesho Mei 10 katika Viwanja vya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema ni bahati kwa mchezo wa Gofu kupata Mgeni Rasmi kutoka Ngazi ya Juu ya Uongozi wa Wizara Husika.

“ Tumekuwa na wageni rasmi Kila Mara Lakini kutoka katika Wizara Husika kupata kiongozi wa Juu ni Fursa itakayowawezesha kuufahamu mchezo na Changamoto zake kwa Ukaribu” Alisema Mweyekiti.

Aliongeza kuwa mashindano haya ni makubwa na  ni moja kati ya mashindano ya ratiba na kusimamiwa naa Chama cha Gofu Tanzania na  Lugalo tumepewa dhamana ya kuyaendesha huku yakijumuisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali.

“ Licha ya kuwa Wazi lakini Klabu tarajiwa ni wenyeji Lugalo, Dar es Salaam  Gymkhana, Arusha Gymkhana, Moshi Gymkhana, TPC Moshi, Morogoro Gymkhana na Mufindi Gofu klabu na wachezaji wengine Wa ndani na nje watakaojitokeza”  Alisema Brigedia Luwongo.

Kwa Upande wake Afisa tawala wa Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule Alisema kutokan na ukubwa wa mashindano Uchezaji Utagawanyika katika makundi matatu kwa kujumisha  Wachezaji wa kulipwa wachezaji wa ridhaa na kwa kuwa ni shindano la wazi, linatoa fursa pia kwa wachezaji wasaidizi (Caddies)

 Aliongeza kuwa  wachezaji Wasaidizi na  kulipwa watacheza siku ya Alhamisi na Ijumaa ya tarehe 10 na Jumamosi na Jumapili kwa Wachezaji wa Ridhaa  na imepangwa kufanyika hivi ili wachezaji wa kulipwa waweze kusimamia mchezo siku zingine za Mashindano.

Kwa upande wake mwakilishi wa TANAPA  Dattomax Sellanyika Alisema Tanapa itaendelea kudhamini na imefanya hivyo kwa mara ya pili ili kutoa fursa nzuri kwa Wadau wa mchezo huu kupata taarifa na kutembelea hifadhi na vivutio  kutokana na kuchezwa na Wageni Wengi.

Naye katibu mkuu wa Chama cha Golf Tanzania Boniface Nyiti aliipongeza klabu ya Lugalo kuwa Chachu ya Mchezo wa Golf na kuwa kivutio cha Wachezaji wengi kufuatia michuano wanayokuwa  wameiandaa.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini