Msanii wa Muziki Bongo, Nandy amesema kuwa mama yake anampenda sana Ruby na anapenda muziki wake.
Kauli hiyo imekuja baada ya wasanii hao kushindanishwa mara nyingi mtandaoni, jambo ambalo Nandy amesema sio kitu kibaya kushindanishwa nae kwasasa msanii huyo ana uwezo.
"Mama anampenda sana Ruby anapenda muziki wake na tunasikiliza sana nyimbo zake, mimi kufanya kazi na Ruby bado hatujawaza japokuwa ni msanii mzuri na itakapofikia hatua ya kufanya kazi tutafanya tu," alisema Nandy.
"Hatujawahi kuwa karibu na namba yake sina, nilikuwa napenda kushindanishwa nae , ukishindanishwa na kitu kibaya ndio utachukia, ukishindanishwa na kitu kizuri inaonyesha na mimi uwezo wangu ni mzuri nilikuwa napenda na naona sawa tu."
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments