Petit Man Aonyesha Machungu Kwa Esma | ZamotoHabari.

Petit Man Aonyesha Machungu Kwa Esma
MENEJA wa wasanii mbalimbali Bongo, Hemed Manungwi ‘Petit Man’ ameonyesha machungu yake ya ndani kwa aliyekuwa mke wake, Esma Khan, baada ya kuona amemblock kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Akizungumza na Za Motomoto, Petit Man alisema kuwa hana budi kumshukuru mkewe huyo kwa kumzalia mtoto lakini alitamani siku ambayo an­amtakia heri ya kuzaliwa mtoto wao huyo kwenye mtandao Esma angeona alichoandika.

“Unajua nilitamani napotoa shukurani mzazi mwenzangu huyo angeona lakini kwa bahati mbaya kaniblock sasa sina jinsi najua watu wake wa karibu watamwambia,” alisema Petit Man.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini