Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amepiga marufuku ukamataji wa vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa na Madini ya dhahabu unaochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo ndani ya Pori la Akiba la Rungwa Wilayani Manyoni, Mkoani Singida kinyume cha sheria.
Serikali imeuagiza Uongozi wa Pori hilo kuhakikisha unaimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayodaiwa kuwa na Madini ndani ya pori hilo ili kuzuia Wachimbaji kuingia na kuendesha shughuli ya uchimbaji wa mchanga kinyume cha sheria.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments