KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa wamejipanga kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Coastal Union mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo leo wataingia kwa mbinu nyngine.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa amejipanga kulipa kisasi kwa Simba kutokana na maandalizi ambayo ameyafanya.
"Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wenye uzoefu ila hilo hainipi taabu kwa kuwa ni timu inayofungika na mbinu zao tayari nimeshazitambua.
"Nimewapa kazi mabeki kuzuia kasi ya mashambulizi ya Simba na pia nimewapa kazi washambuliaji kuliandama lango la mpinzani lengo ni kupata pointi tatu, mashabiki sapoti ni muhimu," amesema Mgunda.
Coastal Union imecheza jumla ya michezo 33 ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 41, Simba ikiwa nafasi ya pili imecheza michezo 30 ina pointi 78.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments