Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa malengo yao msimu huu hayakuwa kushiriki michuano ya kimataifa na hata kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Zahera ameyasema hayo mara baada ya kipigo cha jana dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Kombe la FA.
Pia amedai kwenye ligi malengo yao hayakuwa kubeba ubingwa lakini baada ya kuwa wanacheza na wanashinda wakaamini kuwa wanaweza kubeba ubingwa.
Kocha huyo ameongeza kuwa hawana cha kupoteza kipindi hiki na sasa wanajipanga kwa msimu ujao baada ya kushindwa kuwa mabingwa wa kombe na ASFC.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments