Spika Ashangazwa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Kusimama...Ataka Serikali Kufafanua | ZamotoHabari.


Spika Job Ndugai ameitaka Serikali itakapo kuwa inahitimisha mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, kueleza kwa nini ujenzi wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani haufanyiki licha ya mzabuni kupatikana kutoka nchini China.

Amehoji hivyo, leo Bungeni baada ya Wabunge mbalimbali kuhoji mradi huo wa bandari kukwama wakati wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya mwaka 2019/20.

Amesema kuna wakati alitembelea China na walisema ujenzi wa bandari hiyo ukikamilika utakuwa na tija kubwa kwa nchi kuliko ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway - SGR) unaojengwa, na kushangaa kuwa ujenzi wa reli umeanza badala ya bandari.

Amefafanua kuwa kukamilika kwa SGR bila kuwa na bandari ya kisasa kama hiyo ambayo ilikuwa ijengwe Bagamoyo ni kazi bure kwani mpaka sasa nchini hakuna bandari nzuri hivyo Serikali inapaswa kuliona hili.

Aidha, baadhi ya Wabunge waliohoji kuhusu suala hilo na kuhitaji ufafanuzi ni Hussein Bashe(Nzega Mjini-CCM), Lucy Magereli(Viti Maalum-CHADEMA), Ally Salehe(Malindi-CUF), Charles Tizeba (Buchosa-CCM) na Dkt. Shukuru Kawambwa(Bagamoyo-CCM).

Mwananchi
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini