Spika wa Bunge Job Ndugai amesema ujenzi wa bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ukikamilika utakuwa na tija kubwa kwa nchi kuliko ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaojengwa.
Akizungumza leo Bungeni ameitaka Serikali kueleza kwa nini ujenzi wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo haujengwi licha ya mzabuni kupatikana kutoka nchini China
Amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe pindi atakapokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti yake leo Jioni kutoa ufafanuzi wa suala hilo.
Spika Ndugai amesema hayo leo bungeni ambapo ameeleza kuwa kukamilika kwa reli ya SGR bila kuwa na bandari ya kisasa kama hiyo ambayo ilikuwa ijengwe Bagamoyo ni kazi bure kwani mpaka sasa nchini hakuna bandari nzuri hivyo Serikali inapaswa kuliona hilo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments