StarTimes Kids yatambulishwa shule za Msingi Mchikichini | ZamotoHabari.

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Jumatano hii ilikuwa ni zamu ya Shule ya Msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule hiyo.

Mbali na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani. “Tunashukuru sana kwa ugeni huu wa StarTimes kuja shuleni kuzungumza na wanawafunzi na kuwapatia chachu ya kujifunza zaidi na kuwasaidia kupata msukumo wa kufanikiwa kwenye masomo yao”, alisema Mwl. Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Mchikichini Bw. Amani Levison Kidiala.

“Pia maudhui ya chaneli hii yamewachangamsha wanafunzi na pia itakuwa ni sehemu ya ukuaji wao kwa sababu kuna vitu vingi wanavyoweza kujifunza kupitia vipindi ambavyo vinafundisha sanaa na stadi mbali mbali za kimaisha.” Aliongeza. ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambay wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.

“Vipindi vingine vina mafunzo ya ustadi ambao utawasaidia watoto kujijijenga kiakili na kujiamini zaidi. Lengo letu kuja shule ya Mchikichini ni kwa sababu wanafunzi wa shule hii wanabeba uhalisia wa watoto wengi wa kitanzania”. Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui, StarTimes Tanzania.
Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios akiuliza maswali na kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala(katikati) akitoa shukrani kwa Startimes Tanzania kwa kuweza kuwakumbuka wakati wa kukabidhiwa zawadi ya King'amuzi cha Startimes wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. Kulia ni Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa na kushoto ni Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kulia) akimkabidhi zawadi ya dishi la Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. Kulia ni Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa(kushoto) akimkabidhi dekoda ya Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala(kulia) wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 
Wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule ya msingi Mchikichini wakiangalia iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam wakiangalia katuni zinazopatikana kwenye chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Picha ya pamoja


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini