TAFITI NI MOYO WA TAALUMA KATIKA KULETA MAENDELEO NCHINI-PINDA | ZamotoHabari.


"Atembelea na kujifunza utekendaji wa kazi katika baadhi ya Ndaki na Shule Kuu"


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amesema tafiti ni duru inayotanua mawanda ya taarifa na kuchangia katika kuleta maendeleo nchini na kwenye jamii kwa ujumla. 

Amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Tano ya Tafiti akiwa mgeni rasmi wa wiki hiyo iliyoanza leo katika Chuo Kikuu Dar es Salaam tarehe 6 Mei,2019. 

"Wiki hii itachochea ushirikiano kati ya Chuo Kikuu na serikali na kusaidia kuhabarisha umma kuhusu tafiti zitakazo oneshwa na kuzisikia na jinsi zitakavyosaidia kuleta maendeleo katika jamii", alisema Pinda. 

Maendeleo ya jamii yanahusiana moja kwa moja na maendeleo ya tafiti kwani ukuaji jumuishi wa uchumi katika masuala ya maendeleo huenda sambamba na matumizi bora ya rasilimali, alisema. 

Pinda amepongeza uongozi wa chuo kikuu kwa jitihada ya maboresho katika upande wa elimu kwa kuchagua njia mbadala ya ufundishaji kwa vitendo, amekitaka chuo kutumia vema mfumo huo mpya wa ufundishaji ili kuondoa changamoto zilizopo pale wanafunzi wanapohitimu mafunzo yao kuweza kufikiria kujiajiri wenyewe. 

MAPEMA: Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof. William Anangisye alisema, tafiti hizi huleta maendeleo na ukuaji wa misingi muhimu sana inayochochea katika kuhamasisha uchumi wa viwanda, kwani tafiti nyingi zinatusaidia katika kuongeza thamani za shughuli chuo kikuu kwa ujumla kwakuwa tunazingatia mihimili mitatu ufundishaji, tafiti na elimu, alisema. 

Maonesho ya Wiki ya tafiti ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Jumatatu tarehe 6 hadi Jumatano tarehe 8 Mei 2019 yenye kauli mbiu isemayo "Utafiti kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu" . 

Imetolewa na Afisha Habari na Uhusiano 

Imetolewa na Afisa Uhusiano 
Kitengo cha Huduma kwa Umma 
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam 













Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini