KAMPUNI ya simu nchini, TECNO imedhamini mashindano ya wanafunzi wanaojifunza lugha na tamaduni za kichina katika chuo kikuu cha mlimani kwa kushirikiana na taasisi ya Confucius iliyopo chuoni hapo.
Mashindano hayo yamefanyika katika ukumbi wa chuo uliopo katika jingo jipya la library iliyojengwa kwa udhamini wa watu wa china, yalishirikisha takribani washiriki kumi na mbili ambapo wote walikua ni wanafunzi wa chuo kikuu cha mliman.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo meneja mahusiano, bwana Eric Mkomoye alisema kua TECNO imesaidia kuwapa nafsi vijana wa ktanzania wanaotamni kutimiza ndoto zao kupitia kujifunza tamaduni za nchi nyingine hasa katika kukuza taaluma zao pia kuweza kuwasiliano na watu wa mataifa mbalimbali, aliendelea kwa kusema kampuni yao pamoja na taasis ya Confucius wametoa zawadi mbalimbali ikiwemo simu aina ya spark 3 pia safari ya kwenda nchii china kujifunza zaidi kw awashiriki washindi wawili.
Mashindano ya kuongea kichina katika chuo kikuu cha mlimani hua yanfanyika kwa usimamizi mkubwa wa taasisi ya Confucius iliyoanzishwa mwaka 2013 kwa makubaliano kati ya chuo kikuu cha mlimani na makao makuu ya taasisi ya Confucius yaliyopo Hanban na Zhejiang yakihudhuriwa na makamu wa chuo kikuu cha mlimani Prof. Rutinwa , mkuu wa utamaduni kutoka ubalozi wa China bwana Gao Wei.
Mwaka jana na mwka huu TECNO mobile imedhamini mashindano haya na kuyaboresha kwa kuongeza zawadi kwa washindi, washiriki na hata wahudhuriaji kwa njia ya bahati nasibu,
Kampuni ya TECNO kwa sasa inayotangaza simu yake mpya aina ya TECNO Spark 3 imeeendlea kudhamini matukio mbalimbali yanayohusu jamii hasa katika kukuza vipaji vya vijana wa kitanzania na kufanikisha ndoto zao kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo ile maarufu ya kua shujaa wangu.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments