VODACOM YAHITIMISHA KILELE CHA WIKI YA AFYA NA USALAMA JIJINI DAR | ZamotoHabari.

Emmanuel Mabula wa BestOne Company (shati la grey) akiwaelekeza wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc jinsi ya kutumia kifaa kimojawapo cha umeme katika hafla ya kuhitimisha wiki ya afya na usalama iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inaendelea kutimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba wanafanyakazi wake wapo katika mazingira bora na kuzingatia sheria za afya na usalama makazini.
Acky Charles wa Dartcom Miles (reflector ya kijani) akiwaelekeza wafanyakazi wa Vodacom Tanzania juu ya matumizi ya vifaa mbali mbali vya usalama, katika hafla ya kuhitimisha wiki ya afya na usalama iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampuni hiyo inaendelea kutimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wake wapo katika mazingira bora na kuzingatia sheria za afya na usalama makazini. 
Mkurugenzi wa Rasilmali Watu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Vivienne Penessis (kulia) akimkabidhi cheti cha ushiriki Hilda Ndakidemi wa kampuni ya BMTL katika hafla ya kuhitimisha mwezi wa afya na usalama iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania mapema wiki hii jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inaendelea kutimiza wajibu kuhakikisha kwamba wafanyakazi wake wapo katika mazingira bora na kuzingatia sheria za afya na usalama makazini.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini