Waziri Lugola Atoa Agizo Mkuu wa Polisi Geita Kusimamishwa Kazi | ZamotoHabari.


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwasimasha kazi mkuu wa polisi Geita, mpelezi wa wilaya na mkuu wa kituo cha polisi Geita kupisha uchunguzi kufuatia tukio la kutoroka mahabusu 15 Mei 21 mwaka huu.

Pia ameagiza askari wengine nane waliokuwa wakiwalinda mahabusu hao kuwekwa ndani.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia tukio la mahabusu 15 kutoroka mapema wiki hii Mei 24 wakiwa kwenye jengo la Mahakama ya Mkoa wa Geita walipofikishwa kwaajili kusikiliza kesi zao
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini