Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Esther Samwel (35) mkazi wa Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kuiba nyanya debe moja na nusu, mboga aina ya chinese mafungu sita na mahindi mabichi matatu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Richard Abwao, tukio hilo limetokea Juni 19,2019 majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika maeneo ya Kitangili, kata ya Kitangili, tarafa ya Shinyanga Mjini, Manispaa na Mkoa wa Shinyanga.
“Chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu marehemu kuiba nyanya debe moja na nusu, mboga aina ya chinese mafungu sita na mahindi mabichi matatu", amesema Kamanda Abwao.
Kamanda Abwao amesema juhudi za kuwatafuta na kuwakamata waliohusika na tukio hilo zinaendelea.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments