Muigizaji wa filamu za bongo , Aunt Ezekiel amefunguka juu ya kilio alichoangua na chozi kumtoka wakati alipohudhuria kusikilizwa kwa kesi inayomkabili partner wake in crime, Wema Sepetu mapema wiki hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu.
Wema Sepetu alipatwa na dhahama ya kukaa rumande kwa siku saba kwa kosa la kuidharau Mahakama kwa kushindwa kuudhuria kesi yake ambao inasikilizwa katika Mahakama mara kadhaa bila kutoa taarifa.
Baada ya Wema Sepetu kutupwa lupango kwa siku saba, Aunty Ezekiel aliutumia ukurasa wake wa kijamii kumpa pole kipenzi chake huyo na kumtia moyo kwa kupost picha zenye jumbe mbalimbali.
Wakati wa kesi ikiwa inaendelewa kusikilizwa mapema Jumtatu hii katika mahakama hiyo, Aunty Ezekiel alionekana kushindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio cha kichini chini, na lilionekana ni chozi tu.
Kuhusu kumwaga Chozi
Aunt aliliambia gazeti moja la udaku kuwa, alikuwa akiumia mno kila alipokuwa akimtazama wema akiwa amesimama pale kizimbani kwani alijua lolote linaweza kutokea ama kupewa dhamana au kurudishwa mahabusu.
“Wema ni rafiki yangu ambaye hata nikiwa na shida kiasi gani anakuwa na mimi wakati wote bila kuchoka hivyo kwa nini nisijisikie vibaya ninapomuona na yeye yupo matatizoni? Roho ilikuwa ikiniuma,” alisema aunt.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments