Benki ya Azania yazindua Kampeni Ya ‘AMSHA NDOTO’ kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa Watanzania. | ZamotoHabari.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Itembe Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Amsha Ndoto ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.Kulia kwake ni Mkurungezi wa Biashara wa Benki ya Azania Rhimo Nyansaho na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo mapema leo Jijini Dar es salaam.
Wanahabari wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya AMSHA NDOTO


 Benki ya Azania (ABL) leo imetangaza uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina, ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.

Kampeni itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba 2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti(kwa ajili ya kila mmoja) na Watoto Akaunti(kwa ajili ya watoto tu).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, Ili kustahili kupokea zawadi, wateja wanapaswa kuwa na akiba yenye thamani ya TZS 1,000,000 kwenye akaunti zao na kuendelea ili kuwawezesha kustahili kuingia kwenye fainali ya droo na hatimaye kuweza kushinda. Washindi wa 3 watapatikana kila mwezi. Kupitia kampeni hii wateja wataweza kujishindia mpaka mara mbili ya kiwango walichoweka kwenye akaunti, ambapo kiwango hiki cha zawadi huweza kufikia mpaka Shilingi milioni Tatu

Akiongelea kuhusu vigezo vya washiriki, Itembe alisema kuwa wateja ni lazima waweke akiba ya kiasi cha TZS 500,000 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima, na wale watakaoweka akiba kiasi cha TZ 1,000,000 watapewa tokeni zitakazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho itakayowapata washindi.

“Tunawahamasisha watanzania wote, wateja wetu wa sasa na wapya,wazazi na walezi kufungua akaunti hizi ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuongeza mitaji, kulipia kodi za pango na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye”, alisema Itembe, akigusia pia kuwa akaunti hizi zitakuwa fursa ya kuwahimiza kuweka akiba kwa ajili ya .

Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde,tumuwezeshe ada ya shule’, itawasilishwa kupitia radio na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Google Display placement na tovuti za ndani. ABL pia imetengeneza tovuti ndogo kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitia linki hii: amshandoto.com.

Masharti na vigezo kuzingatiwa




Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini