Diamond afunguka machungu anayopitia kuwasiliana na watoto wake Afrika Kusini “Mobetto muelewa, Zari Kani-block siwaoni watoto” | ZamotoHabari.

Msanii wa bongo freva daimond amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa kwasasa hana uwezo wa kuwaona watoto wake wa Afrika Kusini , Tiffah na Nillan, kwenye mitandao ya kijamii kwani mama yao amem-block asiwaone.



Diamond akiongea na waandishi wa habari leo Jumanne 25, 2019 amesema kuwa kuna kipindi walikuwa wanawasiliana na mzazi mwenzie Zari na kuongea na watoto wake ila kwasasa hata email hajibiwi.

Kwa upande mwingine, Diamond amemsifia mzazi mwenzie wa pili, Hamisa Mobetto kwa kusema kuwa ni muelewa kwani hana usumbufu wowote pindi anapotaka kuonana na mwanae, Dylan.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini