KAMBI MAALUM KWA WANAWAKE WENYE MAKOVU,ULEMAVU ULIOTOKANA NA VURUGU MAJUMBANI AU AJALI KUFANYIKA JUMAMOSI HII KISARAWE | ZamotoHabari.





KISARAWE PWANI Juni, 2019. Programu ya Reconstructive Women and Children ni jitihada ya ushirikiano kati ya Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam (AKHD), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pamoja na shirika la kibinadamu la Reconstructing Women International (International Confederation for Plastic, Reconstructive and Aesthetic Surgery) ili kutoa huduma ya upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile au ngozi iliyokakamaa kwa wanawake na watoto wa kike maskini wenye ulemavu uliosababishwa na ukatili wa majumbani, kuungua na ajali.


 Ushirikiano huu unalenga kubadlishana na kuimarisha utaalamu wa upasuaji kwa ajili ya kushughulikia hitaji la kitiba la upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na Kanda ya Afrika Mashariki. 


Programu hii ilianzishwa mnamo Januari 2016 ikihusisha wapasuaji kutoka Marekani, Canada na Ulaya wakifanya kazi kwa karibu na wanatiba wa Kitanzania. Tangu hapo, kupitia awamu NNE, operesheni 143 za upasuaji zimefanywa bila gharama yoyote kwa wagonjwa (ambao ni wahanga wa ukatili wa majumbani, kuungua na ajali), na kurejesha utendaji wa kimwili na mwonekano wa wanawake na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 


Kwa kuwa upasuaji huu  wa kuboresha maumbile, ngozi iliyokakamaa, umeonesha kuboresha kwa kiwango kikubwa maisha ya wale wanaosumbuliwa na unyanyapaa na ulemavu, Hospitali ya Aga Khan na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinayo furaha kushirikiana kwa mara nyingine tena katika mradi huu wa kipekee. 


Kambi kubwa ya uchunguzi ili kuwatambua wagonjwa wenye uhitaji kwa ajili ya awamu ya 5 Hospitali ya Aga Khan  Muhimbili pamoja na shirika la SADAKA network  Tunapanga kuwa na kambi hii kwa mara ya kwanza kabisa wilayani Kisarawe .kambi hii itafanyika  hospitali ya wilaya ya kisarawe na mganga mkuu wa wilaya ya kisarawe atakuwepo  na kambi hii imepewa Baraka zote na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe 


Ambapo wanawake na watoto wenye ulemavu mbalimbali wanaalikwa kuhudhuria kambi hii ya tathmini ya awali; wataonwa na wataalamu waliobobea katika upasuaji wa Kubadili na Kuboresha Ngozi/Maumbile iliyokakamaa. 



KWA Mawasiliano 


AKH-D: Olayce S. Lotha, olayce.lotha@akhst.org, Simu: +255-717-516-650 


SD ; Viola Julius ,viola.m@sadakanetwork.com , simu : 0763858029



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini