Mantrac Tanzania yaunga mkono sera ya Serikali ya viwanda | ZamotoHabari.

Huku Serikali ikipiga chapuo kwa ajili ya kuwa nchi ya viwanda na yenye uchumi wa kati, Mantrac Tanzania Limited imeweka historia mpya, ikiwa ya kwanza kwenye sekta ya uchimbaji.

Mantrac ndio waliopewa idhini ya kushughulikia bidhaa za Caterpillar nchini Tanzania, wakisambaza na kuhudumu katika mashine za CAT.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Meneja Mauzo wa Mantrac Tanzania, Butwa Sanga, alisema kwamba katika kujaribu kwenda kwa hali ya juu na kasi ya viwanda, kampuni hiyo inayoshughulikia mashine zenye uwezo mkubwa imekuja na chapa mpya ya Caterpillar yenye ufanisi mkubwa na inayookoa muda.

Alitambulisha mashine mpya kuwa ni New Generation Hydraulic Excavator (NGH) Caterpillar itakayoleta mapinduzi makubwa kwenye ajenda ya kuelekea kwenye nchi ya viwanda, kwa sababu ina ufanisi wa hali ya juu, gharama ndogo na inachukua muda mfupi kukamilisha kazi.

“Viwanda havijengwi kwa mkono, vinahitaji mashine zenye uwezo mkubwa kufanya hivyo,  na kwa kutumia mashine hizi mpya za NGH Caterpillar zilizoingia sokoni, tunatarajia kwamba watu waliojipanga kujenga viwanda vipya watapata kile kinachofaa sana kwa kazi hiyo ili kwenda haraka, tofauti na modeli zile za zamani,” alisema.

Bw. Sanga alikuwa akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu yanayokwenda kwa jina la ‘Changamoto ya Mafundi’ ambapo Mantrac inatoa mafunzo kwa mafundi 30 juu ya jinsi ya jinsi ya kutumia caterpillars hizo mpya zenye teknolojia ya hali ya juu.

Alisema kwamba makatapila hayo mapya ya NHG yanapunguza muda wa kazi kwa nusu na wakati huo huo kupunguza matumizi ya mafuta kwa kati ya asilimia 25 na 45 huku yakiongeza tija na uzalishaji.
 Mkufunzi kutoka Kampuni ya Mantrac, Ehab Abdelfatah Mohamed, (mwenye miwani) akitoa maelezo kwa baadhi ya waendeshaji kutoka makampuni tofauti  kuhusu mashine mpya za uchimbaji aina ya Caterpillar,  zinazosambazwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Waendeshaji hao wanahudhuria mafunzo ya siku tatu yaiyoandaliwa na kampuni ya Mantrac Tanzania.  


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini