Mfanyabiashara Apambana na Majambazi na Kuwapora Bunduki | ZamotoHabari.



Mfanyabiashara Cassian Fortunatus (28) mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro amefanikiwa kumnyang’anya bunduki mmoja wa majambazi waliomvamia nyumbani.

Akisimulia tukio hilo Fortunatus amesema kuwa baada ya kufunga duka lake la huduma za kifedha akiwa na mke wake Zuhura Waziri walirudi nyumba na kabla ya kufika mlangoni ghafla walivamiwa na majambazi hao wawili.

Amesema mmoja alikuwa na bunduki aina ya ‘Shotgun Magnum’alifyatua risasi moja hewani na kuwaamuru waweke chini mkoba wenye pesa.

Alieleza kuwa kwa hofu mke wake aliweka chini mkoba wake mdogo uliokuwa na fedha Sh 200,000 pamoja na simu mbili.

Fortunatus amesema yeye aliamua kugoma kuweka chini mkoba mkubwa uliokuwa na fedha alizotoka nazo dukani na ndipo majambazi hao yalipofyatua risasi mbili hewani kwa lengo la kumtisha.

“Baadaye jambazi mmoja aliamua kuchukua ule mkoba wa mke wangu na kukimbia, nikabaki na jambazi mmoja nikipambana naye na wakati wote huo begi langu lenye hela nyingi likiwa mgomboni yule jambazi alipoona namzidi nguvu akakimbia ndipo nilipoanza kumkimbiza na kwa bahati nzuri alianguka chini na nikamkamata nikaanza kumkaba na kumnyang’anya ile bunduki,”amesema.

Alisema kuwa alipambana na majambazi hayo kwa dakika zisizozidi 15 na wakati wa mapambano hayo hakujua kama angefanikiwa kuwanyang’anya bunduki na fedha zake kuwa salama.

Hata hivyo alisema kuwa ujasili huo wa kupambana na majambazi aliupata kutokana na mazoezi anayofanya na kwamba miaka ya nyuma alikuwa akicheza mchezo wa karate.

Kufuatia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbrod Mutafungwa pamoja na maafisa wa polisi wamemzawadia fedha taslimu Sh. 265,000 kwa kuonesha ukakamavu na ujasili uliofanikisha kupatikana kwa bunduki hiyo.

Akizunguzia tukio hilo kamanda Mutafungwa alisema kuwa amemzawadia kiasi hicho cha fedha kwa kuwa kazi aliyoifanya ilipaswa ifanywe na askari aliyepitia mafunzo lakini ujasili aliouonesha ni mfano wa kuigwwa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini