*Hatutasita kukemea washiriki watakaosababisha maungo yao kuonekana kimakusudi.
Na.Khadija seif,Globu ya jamii
MCHAKATO wa kumsaka mlimbwende wa wilaya ya ilala umefunguliwa rasmi jijini Dar es salaam.
Akizungumza na michuzi tv mratibu wa mashindano hayo Lucas Rutainurwa amesema mashindano hayo yamefunguliwa rasmi hivyo warembo wajitokeze kuchukua fomu kwa ajili ya kitambulika kama washiriki katika kinyang'anyiro hicho.
"Fomu zinapatikana na kwa mwaka jana tumefanya mapinduzi mengi mazuri kwani tuliweza kutoa kumi bora ambao walishiriki katika kinyang'anyiro cha nchi (miss Tanzania),"
Hata hivyo ameeleza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwanzo mwa mwezi julai mwaka huu na mshindi wa kwanza atajipatia kitita cha fedha 1000,000 na wapili 5000,00 huku mshindi wa pili
"Vigezo kwa mshindi vipo wazi cha kwanza aweze kupita jukwaani na vazi la ubunifu ambalo halitaweza kuonyesh maungo yake ya ndani, ulimbwende sio kuonyesha maungo ni kupotosha jamii hatutasita kulikemea jambo hilo.
Aidha,ametaja nidhamu ya hali ya juu, ufahamu wa kujieleza ,kuwa na mtanzania vikiwa ni vigezo ambavyo vitaweza kumpa nafasi mlimbwende kushiriki kikamilifu shindano hilo.
Pia ametoa rai kwa makampuni kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwani ni moja ya kuwapa fursa wasichana wakitanzania kujitangaza kimataifa na kuonekana vioo katika jamii na mfano wa kuigwa kupitia kazi za wanamitindo.
Kwa upande wake mshindi wa pili wa mashindano hayo Sheila Rajab amesema kupitia mashindano hayo amejifunza vitu vingi,kuishi na washiriki wengine,kujua tabia zao,kukutana na wabunifu wakubwa mbalimbali.
"Kitu ambacho watu wengi hawafahamu ni kuwa huwezi kufika mlimbwende wa dunia bila kupitia hatua za chini ikiwemo mlimbwende wa wilaya hadi mkoa ",
Aidha amewaomba wasichana wenye vigezo wajitokeze kwa wingi ili kushiriki.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO




0 Comments