Omar al-Bashir Ajitokeza Hadharani kwa mara ya Kwanza Baada ya Mapinduzi ya Kijeshi | ZamotoHabari.

Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa kwake madarakani mwezi Aprili.

Bwana Bashir alikuwa akitolewa gerezani katika mji mkuu, Khartoum kwenda kwenye Ofisi ya mwendesha mashtaka ambaye alimsomea mashtaka ya rushwa yanayomkabili

Akiwa amezungukwa na askari wa usalama, Kiongozi huyo wa zamani mwenye miaka 75 alikua amevaa vazi lake jeupe na kilemba.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa maburungutu ya fedha za kigeni yalikutwa kwenye magunia nyumbani mwake baada ya kuondolewa madarakani alikohudumu kwa takribani miaka 30.

Bashir alionekana akishuka kwenye gari kuingia kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka, akitabasamu na kuzungumza na walinzi, lakini baadae alirejea akiwa na uso usio na furaha, Shirika la Reuters limeeleza.

Bwana Bashir pia anatakiwa na mahakama ya kimataifa, ICC, akishutumiwa kuongoza vitendo vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo la Darfur, shutuma ambazo amezikana.

Wakati huohuo, Mohamed Hamdan ''Hemeti'' Dagolo,ambaye ni makamu wa rais wa jeshi la junta aliahidi kuwafikisha mbele ya sheria watu ghasia za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa upinzani, zaidi ya watu 100 waliuawa tarehe 3 mwezi Juni vikosi vya Sudan vilimaliza maandamano baada ya waandamanaji kupiga kambi makao makuu jeshi wakidai utawala wa kiraia.

Mamlaka ya jeshi la Sudan, limekuwa likikosolewa na mataifa duniani kuhusu namna walivyokabiliana na waandamanaji.

Sudan imeondolewa uanachama wa Umoja wa Afrika.

Siku ya Ijumaa baada ya kutembelea Khartoum,mjumbe wa Marekani barani Afrika, Tibor Nagy ametaka kufanyike uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotekelezwa.

Mazungumzo kati ya waandamanaji na Baraza la kijeshi yalivunjika baada ya ghasia kutokea
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini