Sakata la Lissu: Askofu Bagonza amesema kuna tofauti ya Bunge na bonge
Posted On: June 30, 2019 4:28 Am GMT+0000 Posted By: Beatrice Shayo Comments: 0
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza ametoa kauli yenye fumbo kufuatika sakata la kuvuliwa Ubunge aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook alifafanua tofauti ya Bunge na bonge.
Ujumbe huo wenye kichwa cha habati ‘Kuna tofauti kati ya Bunge na Bonge.’
“Bunge huongozwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni, tamaduni za mabunge, mila na desturi nzuri, busara na hekima.
Askofu Bagonza aliongezea kuwa:”kikikosekana kimoja hapo juu, linageuka kuwa bonge. Maana yake, bonge linatisha, linaonea, linapendelea, linajichanganya, linahujumu, linajihujumu, linalipiza kisasi, linakera na halina utu wala huruma.”
“Bunge letu siyo bonge. Mungu Ibariki Tanzania. Libariki Bunge letu. Liepushe na majaribu ya kuwa bonge.”
Juni 28,2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alisema Lissu amepoteza sifa za kuwa mbunge kwa sababu ya kutokujaza fomu za mali na madeni ya maadili ya viongozi wa umma na kutokutoa taarifa sehemu alipo.
Spika Ndugai alisema hafahamu Lissu yuko wapi na amekuwa akimwona katika vyombo mbalimbali vya Kitaifa na Kimataifa akizungumza masuala mbalimbali huku bungeni akiwa haonekani hivyo kamwandikia barua mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi kumweleza kiti cha Lissu bungeni kiko wazi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments