Sima: Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kuchukua Hatua kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi | ZamotoHabari.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima amesema Ofisi hiyo imeendeelea kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema hayo leo bungeni, Dodoma alipojibu swali la Mbunge wa Konde Mhe. Khatibu Said Haji aliyeuliza je hatua gani Serikali inachukua kudhibiti athari za uharibifu katika Bandari ya Tanga eneo la ‘Deep Sea’ lango kuu la kuingilia na kutokea.

Mhe. Sima alisema Ofisi hiyo imeandaa mkakati na kutekeleza mkakati wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi wa mwaka 2007 na mkakati wa kulinda wa mwaka 2012.Alisema mikakati hiyo inaelekeza hatua za haraka za kulinda sekta muhimu za maji, maliasili, miundombinu, afya, nishati, ukanda wa pwani na maeneo ya bahari.

“Eneo la ufukwe linalojulikana kama Deep Sea lililopo katika Jiji la Tanga linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo athari za kimazingira kama vile utupaji wa taka hasa za plastiki na taka zingine ambazo huletwa na mifereji ya maji ya mvua inayoingia baharini kutoka maeneo mbalimbali ya Tanga hivyo Serikali ikishirikia na imechukua hatua za kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wavuvi kuhusu utunzaji wa mazingira,” alisema Naibu Waziri.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini