TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI WAKATI WA MAONYESHO YA SABASABA | ZamotoHabari.


Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi  kuwa inashiriki maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/06/2019 hadi tarehe 13/07/2019.
Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na mikoa ya jirani mnakaribishwa kutembelea Banda letu lililopo ndani ya banda  la Jakaya Kikwete ili muweze kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na afya ya Moyo.
Huduma tunazozitoa ni upimaji wa magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora,  kuelezea kwa kina huduma zinazotolewa na Taasisi na kutoa Rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitaji kupewa rufaa kwenye Hospitali yetu iliyopo eneo la Muhimbili.
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iko kwa ajili ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na  magonjwa ya Moyo. Wananchi wote mnakaribisha kutembelea Banda letu ili muweze kupata huduma   zetu bila malipo yoyote. Madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo chini ya Prof. Mohamed Janabi watakuwepo  katika banda letu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.  

Imetolewa na:
  
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
28/6/2019


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini