Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi kwa Umma Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA pamoja na kitengo cha polisi makosa ya mtandaoni wamefungua kituo cha pamoja kwa lengo la kuwarahisishia wananchi usajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole Kadri wanavyohitaji kwa mtandao mmoja kusajili zaidi ya laini mbili ikiwa unahitaji laini hizo.
Sambasamba na hilo wageni nje ya nchi kuanzia miezi sita wanatakiwa wajisajili NIDA kwa makazi ya muda huku wale wanaongia na hawezi kukaa muda mrefu watatumia hati zao za kusafiria.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maadhimisho hayo Kaimu Mkuu wa TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Jumanne Ikuja amesema kuwa usajii huo wa kitambulisho cha taifa ni kuondokana na utitiri wa vitambulisho vingi ambapo baadhi ya watu walitumia vibaya kwa kuwa na laini zingine kufanya uhalifu.
Amesema mfumo utakomesha uhalifu licha mtu kuwa na laini zaidi moja katika mtandao Mmoja ukomesha wizi wa mtandaoni kutokana na taarifa zake akifanya uhalifu atafikiwa tu.
Aidha amewata wananchi wanaopoteza vitambulisho vyao kuhakikisha kuwa wanaripoti polisi ili kuweza kurudishiwa vitambulisho vingine katika kuepuka kutumiwa kwenye matukio ya kihalifu.
Mhandisi Ikuja amewasisitiza wananchi kufika katika viwanja vya mnazi ili kupatiwa huduma mbalimbali zinazohusiana na Mawasiliano kwani zoezi hilo ni la wiki moja kuanzia Juni 17- 21 mwaka huu.
Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa polisi Kitengo Cha makosa ya mtandaoni Inspekta Edga Masawe amewatahadharisha wa anchi kuacha kutumia simu ambazo wamezinunua kiholela haswa kutoka kwa watu pamoja na zile wanazoziokota ikiripotiwa ni unachukuliwa kama mhalifu.
Hata hivyo amesema kuwa kupitia maadhimisho ya wiki ya utumishi watatoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria za mtandaoni pamoja na madhara ya matumizi mabaya ya mtandao ikiwemo matumizi ya lugha isiyokuwa na staha na picha zisiokuwa na maadili na maneno ya uchochezi.
Mwananchi akiweka alama za vidole katika kukamilisha usajili wa laini ya simu.
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Jumanne Ikuja akitoa maelezo kwa mwananchi wakati waliotembelea banda lá TCRA katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika utoaji na elimu ya Mawasiliano Pamoja usajili wa laini za simu katika kituo kimoja ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika foleni katika banda la NIDA kufanya Usajili wa kupata kitambulisho cha Taifa.
Huduma za usajili na maelezo yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments