Thadayo Ringo (kulia)Mkuu wa Kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) Rolf kibaja mtaalamu wa maudhui TCRA .
Na.Vero Ignatus, Arusha.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imezindua wiki ya huduma kwa mteja katika chuo cha uhasibu Njiro ikiwa sehemu ya kuielimisha jamii kwa kushirikiana na watoa huduma za simu za mkononi.
Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) amesema dhima ya wiki ya utumishi wa umma imesimama kuhakikisha jinsi gani Taasisi za Umma zinawezesha vijana kujiajiri pamoja na kuangalia muingiliano wa uhamiaji kutoka vijijini kwenda mjini
Amesema kuwa wanaangalia jinsi gani wanaweza kuikumbatia Teknolojia katika kusaidia utekelezaji wa utoaji huduma jumuishi na kuhakikisha kwamba wanajenga utamaduni wa utawala bora.
Amesema katika kuzingatia hayo TCRA ilichagua mikoa 5 ambayo inaadhimisha siku hiyo ambapo ni pamoja na Arusha,Mwanza Mbeya Dar es saalam, Dodoma ambapo wapo kwaajili ya kufanya kampeni ya kusajili watu wanaotumia huduma za simu za mkononi kwa kusajili line zao kwa kutumia alama za vidole .
Ringo ametaja changamoto kubwa wanayokutana nayo ni pamoja na watu wengi kufikiria kwamba zoezi hilo linalengo la kuchuliwa alama za vidole,bali wao wanahakiki taatifa kwa kutumia alama za vidole,ambapo wengi wanasita kujidikisha.
Aidha amesema katika kipindi chote hicho wananchi wanaalikwa kuwatembelea,na wao wapo tayari kujibu maswali mbalimbali ambapo amesema kuwa tangia zoezi hilo limeanza muamko ni mkubwa na amesisitiza kuwa kabla ya kufika disemba watakuwa wameweza kukamilisha zoezi hilo kwa asilimia kubwa.Picha na Vero Ignatus.
Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Njiro wakiwa kwenye foleni ya kuchukua namba ya kitambulisho cha Taifa kwaajili ya kusajili laini kwa mfumo wa Biometric ambapo zoezi hilo limefanyika siku mbili chuoni hapo na siku tatu watakuwa katika soko la kilombero .Picha na Vero Ignatus.
Mmoja wa wafanyakazi kutoka NIDA akinsaidia mteja aliyefika kupatiwa huduma ya kitambulisho cha Taifa.Picha na Vero Ignatus.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments