Na.Vero Ignatus,Arumeru
Vijana wametakiwa kuhakikisha wanarudisha mikopo yote waliyokopeshwa kwenye vikundi vyao ili kusaidia kukuza mfuko wa Wazira na kutoa fursa ya vikundi vingine kukopeshwa.
James Kajugus ni Mkurugenzi wa idara ya vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu, ametoa maelekezo hayo alipokuwa akitembelea vikundi mbalimbali vya vijana katika
halmashauri ya Meru.
Amesema Wizara kupitia mfuko wake wa maendeleo ya vijana ulitoa kiasi cha fedha Milioni 103 kwa halmashauri ya Meru kwa lengo la kukopesha vikundi mbalimbali vya vijana vinavyofanya shughuli za maendeleo na ukuzaji wa uchumi.
“Nashangwazwa sana na taarifa hii ya vikundi vingi vya vijana kupata
fedha za serikali lakini wameshindwa kurejesha na hata Saccoss ya vijana
Meru ambayo ndio inasimamia fedha hizo imeshindwa kuvifuatilia vikundi
hivi ili virejeshe mikopo hii”.
Amesisitiza zaidi juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Wizara kupitia
idara ya vijana mbali na mikopo kuwa ni fursa za kuongeza ujuzi kwa
vijana wabunifu ambao hawajasomea na fursa za mafunzo mbalimbli kwa
vijana.
Akielezea changamoto zinazosababisha vikundi vya vijana kushindwa
kurejesha mikopo Mkurugenzu Mtendaji wa Halmashauri ya Meru bwana
Emmanuel Mkongo, amesema vijana wengi hawaaminiani kwenye vikundi
vyao na hiyo kupelekea vingi kuvunjika au wanavikundi kukimbia na
mikopo hiyo
Pia, amesema kuna hali ya siasa kuingilia ufuatiliaji wa fedha hizi za
mikopo na hivyo kufanya mazingira ya urejeshaji kuwa magumu zaidi na
baadhi ya vikundi vya vijana kuingia kwenye siasa hizo.Aidha, amesema mbali na changamoto hizo bado halmashauri yake kushirikiana na maafisa husika wanaendelea kuhakikisha fedha zotezilitolewa na Wizara na halmashauri zinarejeshwa ili kutoa nafasi ya vikundi vingine kunufaika pia.
Nae mwenyekiti wa kikundi cha Old is Gold Arts group bwana Samola Mloe,
amesema mikopo ya vijana inayotolewa na Wizara imesaidia sana kikundi
chao kukua na mafunzo waliyopewa na halmashauri yamewasaidia pia
kupata masoko kupitia mitandao ya kijamii nje ya nchi.
Bwana Kajugusi yupo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa
lengo la kutembelea vikundi mbalimbali vya vijana na kukagua miradi ya
maendeleo inayofanywa na vikundi hivyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana bwana James Kajukusi(mwenye suti nyeusi)akisisitiza jambo kama anavyoonekana katika picha.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments