Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Malinyi, Lucas Lihambalimu (42)
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Wilbroad Mutafugwa amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Juni 13 saa 8 usiku na uchunguzi uliofanywa umebainika chanzo cha mauaji ni mgogoro wa mashamba
Kufuatia shambulio hilo, Askari walifika eneo la tukio na kukuta kipande kidogo cha chuma chenye umbo la duara kinachotumika katika bunduki zilizotengenezwa kienyeji
Aidha, mwili wa katibu huyo, ulifanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi - #regrann
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments