Timu ya Taifa ya Algeria imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mataifa huru Afrika AFCON baada ya kuifunga Senegal kwa goli 1-0.
Algeria wanabeba ubingwa huo kwa mara ya pili baada ya miaka 29 toka ilivyochukua kwa mara ya kwanza huku Senegal akiwa hajalibeba hata moja.
Mchezo huo ulianza na kasi ilichukua dakika 2 kwa Algeria kuandika goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Baghdad Bounedjah baada ya kupiga mpira na kumgonga beki wa Senegal na kupoteza mwelekeo wa mpira.
Mchezo ulikuwa na kasi kubwa, Senegal wakisaka goli la kusawazisha huku Algeria wakitaka kupata uhakika zaidi wa ushindi kwa kupata goli.
Mpaka mapumziko Algeria walienda vyumbani wakiwa kifua mbele. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na washambuliaji wa Senegal kushindwa kutumia nafasi walizozipata.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Algeria wanatwaa ubingwa kwa mara ya pili baada ya muda mrefu.
Mchezaji Ismael Benaccer wa Algeria amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa AFCON mwaka huu huku Mlindamlango wa Algeria Rais Mbolhi ndiyo Golikipa bora wa AFCON.
Algeria wamefanikiwa kuruhusu nyavu zao kutikishwa mara 2 dhidi ya Nigeria mchezo uliomalizika kwa ushindi wa 2-1 na ule wa Ivory Coast 1-1 ulioamuliwa kwa mikwaju ya penati na wakifunga jumla ya 13.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments