Amuuwa Mwenzake Akimtuhumu Kuiba Panga Tangu 2018 | ZamotoHabari.

Amuuwa Mwenzake Akimtuhumu Kuiba Panga Tangu 2018
Jeshi la Polisi Wilaya ya Lindi linamshikilia kwa mahojiano mkazi waa Kijiji cha Rondo Ntene, Aisha Mshamu (65) kwa tuhuma za kumuuwa mwananchi mwenzake aitwae Zainabu Mikumbi (80) kwa madai alikuwa akimtuhumu kwa wizi wa panga lililopotea 2018.


Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi, ACP Prodansiana Protas amethibitisha kuwepo taarifa ya mauwaji hayo na kutaja chanzo kuwa ni ugomvi uliotokana na Zainabu kupoteza panga lake mwezi Disemba 2018.

"Disemba, 2018 Zainabu akiwa anatoka Shambani kwake njiani alikutana na Aisha Mshamu na kumueleza amepoteza panga lake, kama ataliona ampelekee'amesema Kamanda Protas.

Amesema ilipofika Juni 29 mwaka huu, saa 10:0 Alasiri, Zainabu akiwa na Jembe mkononi alienda mashambani kukata nyasi za kuezekea Nyumba yake, wakati Aisha alikuwa ameenda huko kwa lengo la kuchimba dawa na kuanza ugomvi.

Kamanda huyo wa Polisi amesema katika ugomvi wao huo, Aisha alifanikiwa kuchukuwa Jembe la Zainabu na kumpiga nalo kichwani na Shingoni, ambapo alianguka chini na kupoteza fahamu,ambapo Aisha aliondoka kwenda Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji chao cha Rondo-Ntene na kupatiwa barua kwenda Kituo cha Afya cha Rondo kwa ajili ya kutibiwa.

Amesema wakati Aisha akienda Kituo cha kutolea huduma,Mtendaji huyo wa Kijiji akaagiza askari rngambo kwenda kumkamata Zainabu,lakini wakiwa njiani walikutana na ndugu wa Zainabu amebebwa machela na kumpeleka Kituo cha Afya cha Rondo kwa matibabu kufuatia majeraha aliyoyapata,Zainabu baada ya kufikishwa Kituoni hapo, alibainika kuwa ameshafariki.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini