Baada ya Rais Magufuli kukagua ujenzi wa Cherezo pamoja na ukarabari wa Meli jijini Mwanza siku ya Jumanne Julai 16, 2019 na kubaini baadhi ya makontena yenye vifaa yamekwama bandarini hatimaye yameanza kufika Mwanza.
Rais Magufuli akimpigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Doto james siku ya Jumanne Julai 16, 2019.
Akiwa jijini Mwanza leo Julai 20, 2019, Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Elias Kwandikwa amepokea makontena 10 ya vifaa vya ujenzi huo wa cherezo pamoja na ukarabati wa meli za MV Butiama na MV Victoria.
Malori yaliyobeba Makontena yakiwasili Mwanza leo.
Baada ya kubaini makotena hayo yamekwama Mwanza, Rais Magufuli alimpigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na kumtaka ahakikishe taratibu zote zinakamilika kwaajili ya makontena hayo kufika Mwanza kwa wakati.
Aidha makontena 10 yaliyofika leo Mwanza na kupokelewa na Naibu Waziri Kwandikwa ni sehemu ya makontena 56, ambayo awali yalikuwa yamekwama Dar es Salaam.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments