Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar Balozi Amina Salum akizungumza wakati Siku ya Mwani na Viungo katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Edwin Rutageruka akizungumza katika siku ya mwani na viungo katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wadau wa mwani na viungo wakiwa siku ya mwani na viungo.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema bado bidhaa za viungo na zile zitokanazo na zao la mwani zinazozalishwa nchini hazina ubora stahiki jambo linalosababisha wazalishaji kushindwa kuzipeleka katika masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Aidha imesema mdalasini wa Tanzania unahitajika sana duniani, kutokana na kutokuwa na kiwango cha kemikali na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Kadhalika zao la Iliki linahitajika kwa wingi Pakstani ambapo soko lake kubwa Kimataifa.
Waziri wa Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibari, Balozi Amina Salum Ali alisema hayo jana katika siku maalum ya bidhaa za viungo na mwani katika maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Akizungumza, Waziri Amina alisema kilimo cha mazao ya viungo kina tija na kimekuwa kuwalipa sana na kuhimiza wazalishaji kutumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa zenye ubora.
Alihimiza wazalishaji kutumia teknolojia ya kisasa na kutaka vyombo vya taifa kuangalia teknolojia rahisi ya kutumia yenye kuwasaidia wananchi.
Kadhalika alihimiza kuwepo kwa ubunifu katika kutengeneza bidhaa zinazotakiwa na hata kuwa na vifungashio imara na bora ili kumudu soko la ndani na nje ya nchi.
Aidha alisema gharama kubwa za uzalishaji zinasababisha bidhaa kushindwa kwenda sokoni na kuishauri Mamlaka ya Maendeleo Ya Biashara nchini (Tantrade) kuwezesha wazalishaji hao kufikia viwango vya juu katika uzalishaji na pia kuondoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka alisema zipo fursa mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa za viungo na kuwataka wazalishaji kushirikiana na Mamlaka hiyo ili kuweza kufika mbali.
Alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao sio wakweli wakiahidi kusambaza bidhaa katika masoko ya kimataifa lakini wakiwa hawawezi kufanya hivyo.
Kuhusu ushuhuda wa mafanikio ya bidhaa za viungo, Mengi Sume aliwataka watanzania kwa ujumla kuzalisha mdalasini kwa wingi kwa kuwa unahitajika sana na kemikali kama ilivyo kwa mingine.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments