Akiwa katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es salaam Ndg. Ngemela Lubinga Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kwa niaba ya Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM, amekabidhi baiskeli ya umeme ( Electric Wheelchair ) kwa Kijana mwenye ulemavu ili kuhamasisha moyo wa kujitolea kwa wenye uhitaji.
Akifafanua uamuzi huo wa CCM Ndg. Lubinga amesema Chama kilipokea maombi ya mahitaji ya baiskeli ya watu wenye ulemavu kutoka kwa Ndg. Yusuph Samweli kijana mwenye ulemavu wa miguu ili apate wepesi wakushughulika na shughuli mbalimbali ikiwemo masomo yake ya Sekondari.
"Baiskeli hii imetengenezwa na kiwanda chetu cha ndani, tuvitumie viwanda vyetu vya ndani, watanzania wanaweza na Tanzania ya Viwanda imewezekana" amesisitiza Ndg. Lubinga
Huu ni muendelezo wa utekelekezaji wa kazi za Chama ndani ya Jamii Nje ya chama.
Imetolewa na:
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments