NA YEREMIAS NGERANGERA-NAMTUMBO
Akiongea na wakuu wa idara na vitengo pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana Aden Nchimbi alisema madiwani wamehusika katika kukwamisha stendi ya wilaya ya Namtumbo kutofanya kazi.
Bwana nchimbi alisema kuna maswala ambayo hayahitaji siasa katika kutekeleza kwake lakini hili la stendi ya wilaya ya Namtumbo aliwataja madiwani hasa diwani wa kata ya Rwinga kuwa kinara kukwamisha stendi hiyo isifanye kazi.
Hata hivyo bwana Nchimbi alimtaja aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckness Adrian Amlima kuwa alisimamia stendi hiyo ifanya kazi kwa maslahi ya Halmashauri pamoja na wilaya lakini madiwani hao walikuja juu na kumshambulia katika vikao mpaka stendi hiyo imekwama kutumika huku miundombinu iliyowekwa kwa fedha nyingi za Halmashauri kukaa bila kutumika.
Aidha bwana nchimbi alimwambia katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo Mohamed Mavallah kuwa ipo changamoto ya wadau wa maendeleo kushindwa kuchangia shughuli za maendeleo katika wilaya ya yao kutokana na kutazamwa vibaya na viongozi wa chama na wakifanya hivyo wanaambiwa kuwa wanataka kutangaza nia nawao wanadai hawataki migogoro wanashindwa kutoa misaada hiyo kwa wananchi na kurudisha nyuma shughuli za maendeleo alisema katibu tawala huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Evance Nachimbinya naye alimwambia katibu wa chama cha mapinduzi kupitia kikao hicho kuwa miundombinu ya lazima katika stendi hiyo Halmashauri yake imekamilisha .
Alitaja kuwepo kwa choo ya kisasa ,jengo la mapato,jengo la kituo kidogo cha polisi, kuwepo kwa banda la abiria zuri kusubiria usafiri pamoja na kuwepo kwa huduma ya maji na huduma nyingine ya umeme katika stendi hiyo.
Mohamedi Mavallah katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo alisema hayupo tayari kuona wadau wa maendeleo wanakwama kuchangia shughuli za maendeleo katika wilaya yao kwa kuhofia migogoro na akadai atahakikisha wadau wanaendelea kuchangia shughuli za maendeleo kama kawaida ili kuifanya wilaya iendelee kupiga hatua .
Pia aliwataka viongozi wa chama na serikali kushirikiana bega kwa bega ili kuondoa changamoto zilizopo kwa wananchi na kucheza wimbo mmoja katika kutatua changamoto za wananchi badala ya kupishana kimtazamo wakati wa kutatua changamoto hizo.
Halmashaauri ya wilaya ya Namtumbo kupitia idara ya ardhi ilitenga eneo la stendi ya wilaya ya Namtumbo na kisha kujenga miundombinu ya lazima na kufunguliwa na kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa bwana Amour Hamadi Amour tarehe 10mei 2017 lakini stendi hiyo ilipingwa na waheshimiwa madiwani na mpaka sasa haifanyi kazi iliyokusudiwa na Halmashauri na badala yake magari yanaendelea kupakia abiria katika maeneo yasiyorasmi.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Aggrey Mwansasu mwenye shati jeupe mbele mara baada ya kikao hicho kwisha.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments