Mawaziri Bara, Zanzibar Wasaini Makubaliano ya Ushirikiano | ZamotoHabari




Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe(Katikati) akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za
Utalii,Habari,Utamaduni,Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mhe.Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale na kulia ni Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo (Kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) wakisaini Taarifa ya Ushirikiano baina ya Serikali ya
Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Sekta wanazosimamia leo Julai 02,2019 Jijini Dodoma.Wanaoshuhudia ni Viongozi waandamizi wa wa Jamhuri ya Muungano katika Sekta hizo. 
3.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nicholas William akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za Habari, Utalii Utamaduni,Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika sekta hizo kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe
(kushoto) akizungumza na Wanafunzi na wanamichezo wa shule ya Foutain Gate Academy iliyopo Jijini Dodoma ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kukuza vipaji mbalimbali vya michezo wakati akiwatambulisha Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Ally,Abeid Karume (kulia) na Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kulia) kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipoitembelea shule hiyo leo Julai 02,2019. 
Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akifurahia zawadi ya sabuni aliyopewa na Uongozi wa wa Shule ya Foutain Gate Academy mara baada ya kuitembelea shule hiyo iliyopo Jijini Dodoma leo Julai 02,2019. (PICHA NA SHAMIMU NYAKI- WHUSM). 


Na Lorietha Laurence-WHUSM 


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza sekta za Habari, Utamaduni,Sanaa na michezo ili kuongeza tija. 

Uwekaji wa saini za ushirikiano huo umefanyika leo Jijini Dodoma katika ukumbi wa chuo cha Ufundi Veta, baada ya vikao vya ngazi za wataalam na Makatibu Wakuu wa Wizara husika kuwasilisha taarifa hizo kwa Mawaziri na hatimaye kuridhia tayari kwa ajili ya utekelezaji. 

“Hatua hii ni nzuri na muhimu kwetu katika kuhakikisha tunadumisha na kuhifadhi muungano wa kihistoria ambao ulioasisiwa na waasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere na Shehe Amani Abed Karume” Alisisitiza Dkt. Mwakyembe. Aidha, Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa katika sekta ya habari ni muhimu kwa Shirika la UtangazajiTanzania (TBC) kushirikiana na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ili kuandaa vipindi mbalimbali ikiwemo kipindi cha utalii Safari chaneli. 

“Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii nchini , vyombo hivi vya habari TBC na ZBC vinapaswa kushirikiana kuandaa vipindi vya utalii ili kuitangaza sekta hii nje na ndani ya nchi” Alisisitiza Mhe. Mahmoud Thabit Kombo . Kwa upande wake Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inatangazwa na kuenezwa kuna umuhimu wa kuandaa kanzi data itakayojumuisha wataalam wa Kiswahili ambao watakuwa wakifundisha wageni ndani na nje ya nchi. 

“Tanzania imechangia sana katika kukuza lugha ya Kiswahili na watu wengi
wanapenda kuja kujifunza kwetu ,hivyo naamini kwa kuwa na kanzi data hii
itasaidia sana katika kuwapata watalaam wazuri wa kufundisha lugha hii”. Balozi Ally Abeid Karume. 

Vilevile Mawaziri hao wamekubaliana kuimarisha ushirikano katika sekya ya sanaa kwa kuhakikisha kuwa ifikapo desemba 2019 wanakuwa wamesha andaa kanuni zitakazowawezesha watayarisha wa filamu kutoka nje ya nchi ili kuruhusu utumiaji wa maudhui hayo kwa vyombo vya habari vya serikali.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini