Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imempa siku saba mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wachapishaji wa gazeti hilo wawe wamewasilisha majibu dhidi ya madai ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe anayetaka kulipwa Sh bilioni 10 kwa kuchafuliwa.
Uamuzi huo wa mahakama umetolewa mbele ya Jaji Joaquine Demelo baada kupitia maombi ya wajibu wa maombi ya kutaka waongezewe muda wa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani.
Jaji Demelo amesema kuwa wajibu maombi walitakiwa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani ndani ya siku 21 baada ya shauri kufunguliwa Disemba mwaka jana lakini hawakufanya hivyo ambapo Musiba kupitia Wakili wake Majura Magafu waliomba kuongezewa muda japo wadai walipinga maombi hayo wakitaka yasikubaliwe.
“Mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili imeona kesi ina maslahi kwa umma hivyo ni bora na upande mwingine wakasikilizwa. hatuwezi kusikiliza shauri upande mmoja, kesi hii ina maslahi kwa umma kuna haja ya kuusikiliza na upande wa pili, nawapa siku saba muwasilishe utetezi na hati ya kiapo kinzani,” amesema Jaji Demelo.
Hata hivyo, Jaji Demelo amesema kuwa upande wa waleta maombi kama watakuwa na hoja za kujibu utetezi wawasilishe kabla ya Agosti 8, mwaka huu ambapo shauri hilo la madai litaanza kusikilizwa Agosti 6, mwaka huu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments