Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Waongezeka Hadi Asilimia 3.7% Kutoka Asilimia 3.5%. | ZamotoHabari.

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Waongezeka Hadi Asilimia 3.7% Kutoka Asilimia 3.5%.
Mfumuko wa bei wa Taifa  kwa mwaka ulioishia Mwezi   Juni,2019   umeongezeka hadi asilimia 3.7%  kutoka asilimia 3. 5%   kwa mwaka  ulioishia   Mwezi  MEI,2019.

Hayo  yamesema  leo    Julai 8,2019   jijini  Dodoma  na mkurugenzi wa  Takwimuza  Uchumi  Bw.Daniel Masolwa ambapo amesema  hali hiyo inamaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka  ulioishia mwezi  Juni ,2019 imeongezeka   ikilinganishwa na kasi ya iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mwezi  Mei,2019.

Bw.Masolwa amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa  kwa mwaka ulioishia  Mwezi Juni ,2019 kumechangiwa  kuongezeka  kwa bei za  baadhi ya bidhaa za  vyakula na bidhaa zisizo za  vyakula kwa kipindi kilichoishia Mwezi Juni,2019   Zikilinganishwa  na bei ya bidhaa za mwaka ulioishia mwezi Juni,2018.

Baadhi  ya bidhaa za  vyakula zilizochangia kuongezeka  kwa  mfumuko wa bei   wa Mwezi Juni,2019 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia  3.6%,unga wa ngano kwa  asilimia   4.4%,mtama kwa asilimia 4.9%,samaki wabichi kwa asilimia   27.3%,dagaa kwa   asilimia 16.5%,mafuta ya kupikia kwa asilimia 9.5%,maharagwe kwa asilimia 3.0%,mihogo kwa asilimia    16.6% na viazi mviringo kwa asilimia 18.8%.

Aidha,Bw.Masolwa amevitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei     wa Mwezi Juni,2019 ni pamoja na dizeli kwa asilimia 11.4%,petrol kwa asilimia 4.9,gharama za kulala kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 5.8% na vitabu vya shule kwa asilimia 2.4%.

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni,2019 umeongezeka hadi asilimia 2.3kutoka asilimia 2.2% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2019.

Hata hivyo,Mkurugenzi huyo wa Takwimu za Uchumi Bw.Masolwa amezungumzia mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulkioishia Mwezi Juni,2019 ambapo nchini Uganda mfumuko wa bei     umeongezeka kwa asilimia   3.4% kwa mwaka ulioishia Mwezi     Juni,2019  Kutoka asilimia 3.3% kwa mwaka ulioishia Mwezi Mei,2019 na Kenya  mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Juni,2019 umeongezeka  hadi asilimia 5.70% kutoka asilimia  5.49 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2019. 

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu [NBS]ni Taasisi ya Umma  iliyoanzishwa kwa sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 pamoja na mapitio yake ya   mwaka 2018    na kwa mujibu wa sheria hiyo ,NBS imepewa mamlaka ya kutoa ,kusimamia na kuratibu upatikanaji wa taarifa za Takwimu hapa nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za mfumuko wa bei kwa ajili ya  matumizi ya serikali na wadau wa Takwimu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini