MILIONI 85/- ZA MIZANI KATIKA JIJI LA ARUSHA ZALIWA NA WATUMISHI WASIO WAAMINIFU,MHASIBU AKIMBIA,WAWILI WAKAMATWA | ZamotoHabari.


Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha.

IMEELEZWA kuwa zaidi ya Sh.milioni 85 zimepotea kwa mwezi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokana na baadhi ya wafanyakazi wa Serikali , ambao wamekuwa wakichukua fedha za ushuru wa mizani na kufisadi fedha hizo kwa kuziweka mifukoni mwao badala ya kuzipeleka serikalini .

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Maulid Madeni wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kushutukiza katika mizani ya kupimia magari makubwa iliopo katika eneo la Morombo jiji hapa.

Amesema baadhi ya wafanyakazi wa mizani hiyo wakiongozwa na mmoja wa wahasibu wa halmashauri ya jiji(akamtaja jina) wamehujumu uchumi wa serikali ya awamu ya tano kwa kujitaidi kutakasa mifuko yao nakuacha kujaza mifuko kwa Serikali ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli.

"Kiwango cha ukusanyaji wa mapato kwa sehemu husika ni milioni 2.4 kwa siku na kwa mwezi ni kama sh.milioni 85 kwa mwaka ni kama sh.bilioni 1.2 , sasa kwa maana hiyo kwa mwezi halmashauri inapata milioni mbili laki nane tu mafisadi hawa ambao ni huyu muhasibu pamoja na wakusanya ushuru wanatia mifukoni mwao milioni 85 ,sasa milioni hizo 85 mara miezi 12 ni sh.bilioni 1.2,hii haikubaliki,"amesema Madeni

Aidha amesema kuwa muhasibu huyu amekimbia na haonekani mara baada ya kugundua wametambua mchezo wake,na hivyo Serikali itamtafuta popote alipo maana nyumbani kwake hayupo ,kazini hajatokea na simu zake hazipatikani.

"Popote tutakapomkuta tutamkamata na kumpeleka Polisi ili sheria zifuate mkondo wake ,pia tunapenda kumwambia ajisalimishe yeye mwenyewe kituo kikuu cha polisi Arusha ili atoe maelezo hizo sh.bilioni 1.2 zinapotea namna gani.Muhasibu huyu ndio alikuwa amewapanga wapokea ushuru hawa wa mizani ya Morombo na walikuwa wanampelekea fedha,"amesema.

Amesema kuwa taarifa hizo wamezipata kutokana na mfumo wa mshine za kieletroniki ambazo wanazitumia ambapo alitoa mfano juzi Julai 18 zilikusanywa fedha ndogo sana ambazo ni Sh.540,000 lakini kwenye mfumo wa mapato wa kielotroniki unaonyesha kuna shilingi laki moja na kumi tu.Hii inamaanisha wakusanyaji wenyewe wanaiba na wakimpelekea pia mhasibu naye anaiba na anaingiza kiwango anachakitaka kwa hiyo tulipata taarifa tukasema lazima tuende tukafanye ukaguzi na tuje kuwakamata lakini kwa bahati mbaya mhasibu huyu alijua na akakimbia,"amefafanua. 

Ameoa onyo kwa wafanyakazi wote wenye tabia hii kwani pindi watakapo mpata fisadi au muhujumu uchumi anaeshibisha mifuko yake badala ya kufikisha fedha za Serikali salama atakama mdogo kiasi gani watamfikisha katika vyombo vya sheria maana serikali hii haipo tayari kulea wahujumu uchumi na mafisadi

Kwa upande wake Mchumi wa Jiji la Arusha Anna Mwambele amesema kwa sasa hivi katika Jiji la Arusha wamejipanga kufanya ufatiliaji wa mara kwa mara katika vyanzo vya mapato ,ili kubaini iwapo kuna vyanzo vinahujumiwa.

Ameongeza kuwa tangu waanze kufatilia wamebaini fedha nyingi sana zimepotea, hivyo kuamua kufanya zabuni mbalimbali na kuamua kuwapa wenzao wa Suma JKT ili kuweza kukusanya hayo mapoto.

Na kuziba mianya mbalimbali ya upotevu wa mapato,ili fedha zinazopatika ziwezeshe jiji la Arusha kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi mengine mbalimbali katika Jiji la Arusha na pia kuweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ambapo alisema kwa mwaka huu 2019/2020 wanamalengo ya kukusanya bilioni ishini pointi saba . 

Katika ziara hiyo wakusanya ushuru wa mizani wawili ambao ni Agness Loishie MA Thobias Julius wamekamatwa na kufikishwa kituoni kikuu cha Polisi huku mhasibu wa Jiji la Arusha yeye amekimbia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Maulid Madeni akiuliza Jambo wakati alipofanya ziara ya kushutukiza katika mizani ya kupimia magari makubwa iliopo eneo la Morombo jiji hapa.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini