MISS TANZANIA KUJULIKANA AGOSTI 23 , MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM | ZamotoHabari.


Fainali za Taifa ya Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2019 chini ya uongozi mpya wa Kampuni ya The Look yatafanyika Agosti 23  2019 katika Ukumbi wa LAPF uliopo Makumbusho, maarufu kama New Millennium Tower.

Fainali  hizo zitafanyika baada ya kukamilika kwa mashindano ngazi ya Mikoa na Kanda ambayo bado yanaendelea kwa hivi sasa.
Mashindano hayo ya Mikoa na Kanda yamekuwa na msisimko sana kwa mwaka huu hasa baada ya kuongezeka kwa mikoa ya Songwe, Simiyu,Kagera ,Tanga na Shinyanga ambayo haikuwepo kwa mwaka jana.

Mara baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya mikoa na Kanda, washiriki wote wataanza kambi ya Taifa mnamo Agosti kwa takriban wiki 3 tayari kwa fainali hizo zitakazofanyika tarehe 23 Agosti 2019.

Ikumbukwe kwamba mrembo atakae shinda taji la Miss Tanzania 2019 atawakilisha Nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia ambayo mwaka huu yatafanyika London Uingereza tarehe 14 Disemba 2019. Aidha kampuni ya The Look inapenda kutoa hamsa kwa watanzania kuudhuria mashindano ya Dunia ili kuongeza motisha kwa muwakilishi wetu. Wale wote watakao penda kuudhuria mashindano ya Dunia wawasiliane na uongozi wa The Look kwa taarifa zaidi.
Mwandaaji wa Miss Tanzania Basila Mwanukuzi na Nelly Kazikazi Miss Tanzania no 2 -2018. wakionesha ngao Crown atakayovalishwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati walipotangaza tarehe ya kufanyika kwa fainali za shindano hilo leo jijini Dar es salaam.
Nelly Kazikazi Miss Tanzania namba mbili -2018 akizungumza katika mkutano huo huku muandaaji wa shindano la Miss Tanzania Basila Mwanukuzi akisikiliza.
Mwandaaji wa Miss Tanzania Basila Mwanukuzi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwananyamala wakati alipotangaza tarehe ya kufanyika kwa fainali za shindano hilo leo jijini Dar es salaam kulia ni Nelly Kazikazi Miss Tanzania no 2 -2018.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini