Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ameshiriki katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) cha mkoani Mwanza.
Kwenye hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo ambapo Rais mstaafu ameiomba serikali kuweka mazingira yenye uwiano sawa wa utoaji wa elimu kwa vyuo vikuu vya umma na vile vya binafsi ili kuepusha dhana potofu kuwa vyuo vya umma vinathaminiwa zaidi.
Pia Rais mstaafu Mkapa ameiomba serikali kufanya mapitio ya mara kwa mara ya sera ya elimu ya juu ili kuendana na hali halisi ya muda husika kwa kuwa vyuo hivyo ni njia ya kuwandaa viongozi wa taifa hili.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments