MRADI WA MAJI MKURANGA KUHUDUMIA WAKAZI 25,500 UTAKAPOKAMILIKA | ZamotoHabari.

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA wamekabidhi vifaa vya mradi wa usambazaji maji wa Mkuranga utakaohudumia wakazi 25,500 sawa na asilimia 83.

Akielezea kwa kifupi mradi huo, Mhandisi John Kirecha amesema, wameshamkabidhi mkandarasi na tayari kuanzia kesho ataanza kazi ya ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita Milioni 1.5

Amesema kuwa, mradi huo utakapomalizika utahudumia wakazi 25,500 ambapo kwa sasa jumla ya wakazi 4500 sawa na asilimia 17.6 ndiyo wanaopata maji safi na salama.

Kirecha amesema, tayari vifaa vimeshafika katika na vingine bado vinaendelea kuja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa tanki na ulazaji wa mabomba yatakayosambaza maji kwenye maeneo ya mradi yaliyoanishwa kwenye mradi.

"Mradi huu utakuwa ni wa km 63, na kukamilika kwa mradi huu kutakamilisha asilima 83 za wakazi waliobaki watakaofaidika na huduma ya majisafi na salama,"amesema Kireche.Ameeleza, mkandarasi ataanza kazi kesho ya ujenzi wa tanki, kituo cha kusukuma maji (booster pump), ulazaji wa bomba kuu na mabomba ya usambazaji maji.

Kwa upande wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalllah Ulega amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuidhinisha na kupeleka mradi huo katika Jimbo lake sambamba na DAWASA kuja kujenga miundo mbinu itakayowawezesha wananchi kupata maji safi na salama.

Ulega ameeleza kuwa, kwa sasa wananchi wa Mkuranga wanaenda kuondokana na kero ya maji ila amewaomba DAWASA kuangalia na vile vijiji ambavyo vipo karibu na mradi unapoishia kupeleka maji ili nao wanufaike kwa kupata maji safi na salama.

Mradi wa Mkuranga ni moja katika ga miradi sita mikubwa iliyosainiwa juma lililopita na tayari mkandarasi ameenda kwenye eneo la mradi kwa ajili ya kuanza kujenga na kukamilisha kwa wakati.

Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni Mkuranga A, Mkuranga B, Viguza, Mgawa, Njia nne, Bigww, Mkalia kitumbo, Uyoyo na Dundani.
 Mhandisi John Kirecha kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA akimuonesha mabomba ambayo tayari yameshawasili kwa ajili ya Mkandarasi kuanza ujenzi wa mradi wa Mkuranga utakaohudumia wananchi 25,500.
Mhandisi John Kirecha kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA akimuonesha mchoro wa ramani ya mradi wa maji utakaohudumia wananchi wa Mkuranga.

 Mhandisi John Kirecha kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA akielezea kwa ufupi mradi wa maji wa Mkuranga utakaohudumia wakazi 25,500.
 Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalllah Ulega amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuidhinisha na kupeleka mradi huo katika Jimbo lake sambamba na DAWASA kuja kujenga miundo mbini itakayowawezesha wananchi kupata maji safi na salama.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini