NCHI 100 KUSHIRIKI SHINDANO LA KIMATAIFA LA MISS UTALII TANZANIA (MISS TOURISM Tanzania INTERNATIONAL) | ZamotoHabari.

Washiriki zaidi ya 100, wenye mataji ya kitaifa kutoka nchi 100 duniani kote watashiriki shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019 / 2020,litakalo fanyika Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2020. 

Kitaifa fainali hizo zitaanzia katika ngazi za kanda maalum za Miss Utalii Tanzania, zitakazo shirikisha washindi wa mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani, ambayo imegawanywa katika kanda maalum nane za mashindano haya. Kanda hizo na mikoa yake katika mabano ni Miss Utalii Kanda ya Kaskazini “Miss Tourism Northern Zone” (Manyara, Arusha, na Kilimanjaro), Miss Utalii Kanda ya Kusini “Miss Tourism Southern Zone“ Ruvuma, Lindi, Mtwara, na Morogoro),Miss Utalii Kanda ya Pwani ya Kiswahili “Miss Tourism Swahili Coast Zone” (Coast, Dar es Salaam and Tanga),Miss Utalii Kanda ya Magharibi “Miss Tourism Western Zone” (Kigoma, Tabora and Katavi),Miss Utalii Kanda ya Ziwa “Miss Tourism Lake Zone” (Kagera, Mwanza, Mara, Geita na Simiyu), Miss Utalii Kanda ya Kati “Miss Tourism Central Zone” (Dodoma, Singida, na Shinyanga, Miss Utalii Kanda ya Nyanda za Juu Kusini “Miss Tourism Southern Highlands” (Mbeya, Rukwa, Iringa, na Njombe), Miss Utalii Kanda ya Mashiriki “Miss Tourism Eastern Zone” (Unguja and Pemba). 

Nchi zote duniani zitakazo shiriki katika shindano hili, zita wakilishwa na warembo wenye mataji ya mshindi 1 au 2 au 3 katika moja ya shindano la kitaifa la nchi husika. Ambapo washiriki wa nje watawania taji la Miss Tourism Tanzania International, na washiriki wa ndani watawania taji la Miss Tourism Tanzania. Mshindi wa taji la Miss Tourism Tanzania International, majukumu yake itakuwa ni ya kimataifa ya kutangaza na kuhamasisha utalii, uwekezaji na utamaduni wa Tanzania kimataifa ,huku mshindi wa taji la Miss Utalii Tanzania ,atakuwa na jukumu la kitaifa la kuhamasisha na kutangaza utalii, mazingira,uwekezaji,huduma za Misitu, Wanyamapori na utamaduni kila mwaka. 

Fainali hizo za kimataifa za Miss Utalii Tanzania, zitakuwa ni tukio kubwa la Utalii na kitamaduni duniani, litaonyeshwa na kurushwa mbashara (LIVE) duniani kote kupitia Televisheni na mitandao ya kijamii, na kutazamwa na zaidi ya watazamaji 750 milioni duniani kote. Wakati wa shindano hili inatarajiwa, zaidi ya wageni 1500 toka nje watakuja nchini kushudiwa fainali hizi, wakiwemo wapenzi wa mashindano ya urembo wa kitalii, waandishi wa habari wa kimataifa, Ndugu na jamaa wa washiriki, watu mbalimbali mashuhuri duniani n.k. 

Washiriki kutoka kila nchi watambatana na waandishi wa wa habari za Televisheni, Mitandao ya kijamii na magazeti ya nchi anayo toka, lakini pia Ndugu jamaa na marafiki. Wakiwa kambini nchini, washiriki wote wakiambatana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa wata tembelea vivutio mbalimbali vya utalii, utamaduni, uwekezaji, mazingira, huduma za misitu, Wanyama pori, maeneo ya wadhamini na ya vipaumbele vya nchi na serikali huku wakipiga picha za Televisheni,Filamu,Magazeti,Majarida na Matangazo. 

Kufanyika kwa shindano hili la kimataifa nchini ni Matokeo ya mageuzi na mapinduzi ya tuliyo fanya ya sanaa ya urembo nchini, ambapo sasa nchi itanufaika kwa kuwatumia washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani kama bango la kujitangaza , lakini pia ni fulsa kwa Tanzania kama nchi, na wafanya biashara kama wadhamini kujitangaza kimataifa na kitaifa kitalii, kitamaduni, kiwekezaji, kiuchumi na kijamii, kupitia washiriki na matangazo mbashara ya Televisheni, Mitandao ya kijamii na machapisho mbalimbali. Lakini hii itakuwa ni fulsa pia kwa nchi, wafanya biashara na wajasiriamali wa Tanzania kufanya mauzo ya bidhaa zao, lakini pia kupenya na kupanua Masoko ya bidhaa zao kitaifa na kimataifa, kwani washiriki na wageni wote wakiwa nchini watatumia huduma na bidhaa za Tanzania kwa Mahitaji yao ya kila siku kwa muda wote watakapo kuwapo nchini. Katika hatua za awali tayari washiriki kutoka nchi mbalimbali za Ulaya, Amerika, Asia, Afrika, Canada na India zimethibitisha kushiriki fainali hizi za kimataifa za Miss Utalii Tanzania ,ambazo zitakuwa zina fanyika kila mwaka nchini. 

Shindano la Miss Utalii Tanzania limeruhusiwa kufanyika tena nchini ,baada ya kufunguliwa na BASATA 22,Januari 2019,baada ya kusitishwa kwa muda baada ya tathmini ya mwaka 2013, kwa lengo la kuboresha zaidi mfumo wa uongozi na wa mashindano, kutoka kwenye mfumo wa kiimla kuja kwenye mfumo mpya wa sasa wa kitaasisi. 

Shindano hili ambalo kwa mfumo mpya sasa linakuwa ni la kimataifa, lina baki kuwa ndilo shindano pekee nchini lenye mafanikio makubwa hasa kimataifa. Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa ndilo shindano la kwanza nchini kabla na baada ya kutwaa taji la dunia, ambapo Miss Utalii Tanzania 2004, Witness Manwingi alitwaa taji la kihistoria la Dunia la Miss Tourism World 2005 – Africa katika fainali za dunia zilizo fanyika Harare Zimbabwe 25-2-2005. Miss Utalii Tanzania ndilo shindano pekee nchini, ambalo limetwaa mataji katika mashindano yote ya Dunia na kimataifa tuliyo shiriki, ambapo hadi sasa tunashikilia mataji 5 ya dunia na kimataifa. 

Mafanikio makubwa zaidi ni pale tulipo andika historia kwa Tanzania kuwa wenyeji wa fainali za dunia za Miss Tourism World 2006,fainali ambazo zilifanyika nchini 11-3-2006 Ubungo Plaza Dar Es Salaam, na kushirikisha nchi 119 duniani, huku fainali hizo zikirushwa LIVE Duniani kote kupitia Televisheni, na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 650 duniani kote. 

Tafiti mbalimbali duniani zimethibitisha kwamba katika mashindano ya urembo, nchi wenyeji wa shindano ndio hunufaika kwa kuwatumia washiriki kutoka nchi mbalimbali kama mabango ya kutangaza nchi mwenyeji, na kuacha nchi shiriki bila faida yoyote ya kimantiki ya kwenda kushiriki au kutuma wawakilishi. Tuna amini wakati sasa umefika, tena wakati sahihi kwa Tanzania na watanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazo nufaika kwa kuwa wenyeji wa mashindano na matukio ya kimataifa ya sanaa ya urembo na mitindo,ikiwa ni tafsiri ya vitendo ya sera za Taifa za Utalii,Michezo,Utamaduni,Wanyamapori,Mazingira,Uwekezaji na Mambo ya Nje. 

Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha – Utamaduni ni Uhai wa Taifa (Miss Tourism Tanzania The Symbol of National Heritage – Tourism is Life – Culture is Living).


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini