P Diddy Ajiingiza Kwenye Uhusiano Mpya na Mpenzi wa Mtoto wake? | ZamotoHabari.



Stori kubwa ambayo imeviteka vyombo vya habari nchini Marekani ni kuhusiana na mkongwe wa muziki wa Hip Hop P Diddy ambaye anadaiwa kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Lori Harvey(22) ambaye ni mtoto wa mtangazaji maarufu Steve Harvey.

Inaripotiwa kuwa mwanadada aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Justin Combs ambaye ni mtoto wa P Diddy ingawa stori ya penzi kati ya Diddy na Lori hazijathibitishwa lakini kwa upande mwingine zimepamba moto baada ya Lori kuonekana akiwa na Didy  kwenye gari aina ya Chauffeured Maybach na kuelezwa kuwa walikuwa wakienda kupata chakula cha jioni (dinner).



Kwa mujibu wa mtandao wa Rap Up uliwahi kuripoti kuwa mwanadada huyo aliwahi kuvalishwa pete ya uchumba na Diddy kitu ambacho hakijathibitishwa mpaka leo na imeripotiwa kuwa penzi kati ya Justin Combs na Lori lilivunjika.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini