Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo Julai 18,2019 wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
Mhe.Magufuli amesema baadhi ya wafungwa wamekuwa wakifungwa kwa kusingiziwa hivyo ni wakati sasa Umefika Kwa Wizara kupita kila gereza na kuchunguza uhalali wa kifungo ili kila mtu apate haki yake kwani serikali ya awamu ya tano ni Wanyonge.
Hivyo ,Rais Magufuli amesema serikali yake hawezi kutawala kwa kuonea watu wanyonge huku pia akisisitiza Umuhimu wa viongozi wa dini kuliombea taifa la Tanzania .
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekumbusha Umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii huku akisema asiyefanya kazi na asile na Serikali yake haiwezi kugawa chakula kwa mtu Mzembe.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments