Serikali Imetoa bil 1.2 kwa Vikundi 561 vya Wanawake, Vijana na Walemavu Njombe | ZamotoHabari.

Serikali imetoa bil 1.2 kwa vikundi 561 vya wanawake, vijana na walemavu Njombe
Serikali mkoani Njombe imesema imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya bil 1.2 kwa vikundi 561 vya wanawake ,vijana na walemavu katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambayo hutolewa kila mwaka na halmashauri kutokana kwenye asimilia 10 ya mapato ya ndani.

Akizungumza katika kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe mkuu wa mkoa huo Christopher Olesendeka amesema serikali imeendelea kurahisisha mazingira ya wajasiriamali na biashara kwa ujumla kwa kuendelea kuhamasiaha uwekezaji na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kukuza mitaji yao.

Mbali na mikopo Olesendeka pia amesema katika mwaka wa fedha ulioisha juni serikali imefanikiwa kutekeleza ilani ya chama katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara zote zinazounganisha wilaya , maji, elimu pamoja na utoaji wa fedha na miradi kwa kaya masikini kupitia mpango wa TASAF hatua ambayo imehimarisha huduma na maisha kwa wakazi wa Njombe.

"Kwa upande wa wanawake ndio waliochangamka sana kuchukuwa mgao wao,jumla ya sh.milioni770,64 elfu na 91 imechukuliwa na vikundi vya akina mama vipatavyo 394,tumejitahidi kuwanyang'anya wapinzani ajenda na ukiangalia kwenye hotuba yangu kwa mkoa wa Njombe zaidi ya bil.480 imetengwa kwa ajili ya miradi mikubwa ya barabara ya kuunganisha wilaya zetu na makao makuu ya mkoa"alisema Olesendeka

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala ameagiza viongozi na wanachama wote kujipanga ili kiweze kuibuka kidedea.

"Serikali za mitaa tukifanya vizuri basi 2020 tutafanya vizuri zaidi, kwa hiyo niwatake wote jinsi tulivyoagizana kila mmoja akatekeleze kwa umakini anavyotakiwa akatekeleze"alisema Mwamwala

Katika kikao hicho pia wametambulishwa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Fakih Lulandala na Nelson Kyando aliyekuwa katibu wa ACT akitokea CHEDEMA ambao wamejiunga na chama cha mapinduzi hivi karibuni.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini