Mkongwe wa muziki wa hiphop duniani 'uncle' Snoop Dogg, ameonekana kuwapigia debe timu ya taifa ya soka la wanawake ya Marekani, kwa kutaka walipwe pesa nyingi baada ya timu hiyo kuchukua ubingwa wa dunia kwa upande wa wanawake.
Staa huyo ameeleza kusikitishwa kwa utofauti kwenye usawa wa kulipwa pesa kwa wanasoka wa kiume na wanasoka wa kike, na yeye ametaka wanasoka wa kike walipwe pesa nyingi zaidi kama wanasoka wa kiume baada ya kuchukua ubingwa huo.
“Hongera ziwaendee timu ya soka ya wanawake kwa kuchukua ubingwa wa dunia kwa mara ya nne , ninachotaka mimi sio kulipwa milioni 206 kwa kila mchezaji, ila kama wanaume ndio wangechukua ubingwa huu wangepata bilioni 1 kwa kila mchezaji, hii sio sawa walipeni tu pesa zao kama mnavvolipa wachezaji nwa kiume. Yaani haiwezekani washinde ubingwa wa dunia halafu wapate kidogo”, amesema 'Uncle' Snoop.
Timu ya taifa ya wanawake ilichukua ubingwa wa kombe la dunia baada ya kuwafunga timu ya taifa ya wanawake wa uholanzi magoli 2-0 na kushinda ubingwa wa nne wa kombe la dunia la wanawake.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments