Baada ya tamasha la Castle Lite unlocks kutekwa na Cloudsfm huku kituo hicho kongwe cha burudani kikimteka msanii aliyekuwa Tamaduni music Wakazi vita kali imeibuka kati ya msanii huyo na rafiki yake Nikki Mbishi.
Wiki hii huko twitter kulikuwa hakutoshi, vijembe, masimango na majibizano yalitawala baina ya wasanii hao wawili yaani Wakazi na Nikki Mbishi. Nikki Mbishi amekuwa akimtuhumu Wakazi kuwa ndiye aliyekwenda kumzibia riziki kwa waandaaji wa tamasha la Hiphop la Castle Lite Unlock. Kwa mujibu wa Nikki Mbishi Wakazi aliwaambia waandaaji kuwa Nikki Mbishi anahitaji pesa kubwa mno hivyo msimchukue.
Kwa upande mwingine tofauti na awali hivi sasa tamasha hilo litalofanyika Jumamosi ya tarehe 20 July 2019 limehodhiwa na cloudsfm hasa Adam Mchomvu.
Washiriki wa tamasha hilo mpaka sasa ni Mr blue, Nikki wa pili, Joh makini, AY, Mwanafa na wengineo.
HALI ILIVYOKUWA HUKO TWITTER
Nikki Mbishi tar 14 July alitweet
"
Jul 14
" ukanda wao kwenye Hip Hop na umatabaka hawakuwahi kutaka kudeal na upande mwingine ila anatokea MDWANZI mmoja anajitia KANDA MAALUM halafu mwishoni anahama ukanda wake kwa ajili ya SHOBO...Madai yake kakamata FURSA. "
Wakazi akatweet kumjibu Nikki Mbishi
"Jul 15
The perpetual habit of playing the "blame game" and looking for a scapegoat in your own shortcomings, has never been known to improve your position nor increase your ability to perform better. Change starts with the "Man in the Mirror" and that's You. #workethicpic"
Nikki Mbishi akapost
"
Wakati unasema natafuta "SCAPE GOAT" Unapaswa ujue wewe ndio wa kwanza kutafuta huo upuuzi uliosema na wewe ndiye uliyeenda kusema kuwa UNJU anataka hela nyingi mtoeni kwenye LIST. Wasanii wote uliyowaletea udalali washaripoti kweye kamati ya MASELA. NANI?"
Jul 15
Ukitoa PRICELESS na KANDA MAALUM ambazo zote nimeshiriki,huyo jamaa yenu anaenda kuimba nini? Mnafiki wa KARNE. Hata aibu hana kazi tufanye wote baadae akawe mwanga mfunga fursa kisa hao waliompa mchongo anashinda nao. @Nashemceetupe kidogo wewe alikwambia nini huyu MMAREKANI?
Jul 15
Nikki anaendelea
@onetheincredibl kaomba kikao cha wasanii wa HIP HOP na marehemu Ruge,mbeleni ONE kawekwa kando mchongo akaushika DALALI wa wasanii na hata FIESTA alienda yeye hakuna cha One wala mpuuzi gani gani? Eti anatumwa kutuuliza SISI THE TRIO tunaperform kwa sh ngapi NikkiZohan
Jul 16
Eti BILINGUAL BEAST wakati kila siku unabite mistari ya wanyamwezi ambao mambugila wa kibongo hawajui ni ya nani Unaweza kuishi CHICAGO lakini suala la Bilingual rap usimuweze@onetheincredibl hata kidogo...KAJINOE Ulikubidi uwe GROUPIE kwetu ili Bongo ikuzingatie. #TM
Jul 16
Wasanii wote hatuna UPEO ila yeye ndiye ana UPEO anajua sana na ana CONNECTION na maboss ili awe MTU WA KATI. Eti oooh majina yenu yametajwa kwenye list ya wasanii FIESTA ila kunafigisu sana na jamaa mmoja ndiye aliyekata majina ya SISI THE TRIO(Jina kapuni)
MAJIBU YA WAKAZI
Webiro N Wassira
wakazi
Spending TODAY by complaining about YESTERDAY, won't help make TOMORROW better. And be careful what you say to somebody today, because you may not have tomorrow to take it back.
NIKKI MBISHI AWASHANGAA AY NA MWANAFA
Nikki Mbishi amesema haamini kama Mwanafa na AY wamekubali kuperform kwenye tamasha la Castle Lite unlocks kwa bei ambayo hata mimi kajamba nani nimeikataa.
SALAMA NA MWANAFA WAMJIBU NIKKI MBISHI
Salama Jabir akatweet "epuka sana mtu anayegombana karibu na kila mtu" tweet ambayo Wakazi, Mwanafa na AY waliiretweet
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments