Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha
Watanzania wametakiwa kujivunia vitu tulivyo navyo pamoja nakujijengea tabia ya kupenda tamaduni zetu na kuacha kubabaikia tamaduni zakizungu kwani tukizitumia vyema tamaduni zetu vyema zitageuka kuwa fursa na kutupatia kipato.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa tamasha la utamaduni lijulikanalo kwa jina la Yakwetu Japhet Jackson alipokuwa anaongea na waandishi wa habari jijini hapa wakati alipouzuria katika usiku wa kumsaka mrembo wa Arusha.
Alisema kuwa Tanzania inamakabila 126 na makabila hayo yote yanatamaduni zao na vyakula vyao ambavyo tukienzi ni vivutio tosha kwa wageni hivyo ambavyo vitatuingizia kipato.
"unajua kuna fursa mbalimbali katika mila zetu na tamaduni zetu iwapo tukizienzi ,watu wanaacha asili yao wanataka kuwa wazungu ,watu wangeishi maisha yao na kuacha kuiga watu wengine wangekuja kujifunza tamaduni zetu na tungepata pesa ,watuwangekuja kutengeneza sinema kupitia mila zetu na tamaduni zetu "alisema Japhet
Aidha pia alisema kuwa yeye katika kuenzi utamaduni ameaandaa tamasha ambalo linatarajiwa kufanyika Aguast 26 jijini Dodoma na itashirikisha makabila yote yaliopo hapa nchi ,ambapo watakuja katika maonyesho hayo na kuonyesha tamaduni zao ikiwemo ngoma zao,mavazi yao pamoja na vyakula vyao.
Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo lililobeba jina la Yakwetu kuona tamaduni mbalimbali za makabila pamoja na vyakula pia alisema mbali na hivyo kutakuwa na mbio zijulikanazo kama Kondoa Irangi marathon itakayofanyika siku ya kilele cha Tamasha hilo.
Mkurugenzi wa tamasha la utamaduni lijulikanalo kwa jina la Yakwetu ,Japhet Jackson
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments