Kufunguliwa kwa miundombinu hiyo kumetoa fursa pana kwa wawekezaji kutembelea maeneo ya uwezekaji yaliyoainishwa na TANAPA na kuwarahisishia watalii kutembea hifadhini.
Akielezea hatua zilizotekelezwa tangu hifadhi zitangazwe rasmi, Mhifadhi Mwandamizi Kitengo cha Ulinzi kwenye hifadhi hizo tatu, Upendo Massawe amesema ufunguzi wa miundombinu zaidi unaendelea kufanywa.
“Kwa sasa hata mwekezaji akija anaweza kutembelea maeneo yaliyohifadhiwa na kuchagua angependa kuwekeza eneo gani.
“Hifadhi ya Burigi-Chato tumefungua Kilometa 218 na kwa Hifadhi ya Ibanda-Kyerwa na Rumanyika-Karagwe tumefungua Kilometa 30,” alisema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, amesema kazi kubwa ya kufungua barabara na viwanja vidogo vya ndege inaendelea.
“Kufungua miundombinu hasa Hifadhi ya Rumanyika-Karagwe na Ibanda-Kyerwa bado ni kazi kubwa, juhudi zinazofanywa sasa ni kuunganisha barabara zinazoanzia njia kuu pamoja na zile za ndani,” amesema Kanyasu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments